Quantcast
Channel: Fadhy Mtanga
Viewing all articles
Browse latest Browse all 76

Nimekaribishwa Nepal kwa vitabu

$
0
0

NIMEPITA duka la vitabu usiku huu hapa Kathmandu, Nepal. Nimekutana na kitabu cha Siddhartha kilichoandikwa na Hermann Hesse. Hesse ni miongoni mwa waandishi, washairi na wachoraji maarufu katika karne ya 19 na 20. Mwanafasihi huyu, mzaliwa wa Ujerumani mwenye asili ya Uswisi, alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel katika Fasihi mwaka 1946.

Simulizi ya Siddhartha ilitolewa mwaka 1922. Kwenye simulizi hii, Hesse anasimulia juu ya safari ya kiroho ya Siddhartha wakati wa Gautama Buddha.

Neno Siddhartha, ni muungano wa maneno mawili katika lugha ya Sanksrit. Sanksrit ni lugha kuu katika Uhindu na Ubudha. Lugha yenye utajiri wa maandishi ya kifalsafa, kiroho na ushairi.

Neno Siddhartha linamaanisha 'siddha' (kupata) na 'artha' (unachokitafuta). Hivyo, Siddhartha inamaanisha mtu aliyeyafikia malengo yake. Ni simulizi ya Siddhartha kutoka Nepal anayeondoka kijijini kwao kwenda kutafuta mwangaza wa kiroho akiambatana na rafikiye mkubwa, Govinda.

Nimekisoma kurasa chache sana. Ninatumai nitakisoma baada ya kummaliza Jackie Collins katika The Power Trip (sikuweza kukimaliza jana kama nilivyokusudia).

Nadhani, nikijumlisha na uelewa nilioupata mwaka 2013 baada ya kumsoma Robin Sharma katika The Monk Who Sold His Ferrari, Siddhartha, itanipanua pia upeo wangu juu ya kupata unachokitafuta.

Alamsiki.

Kathmandu, Nepal. 
Jumatatu, Januari 9, 2017.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 76

Trending Articles