Hapa ni Airpoint, mahali ambapo barabara ipo juu kuliko barabara zote nchini. Eneo hili lipo barabara ya Chunya nje ya jiji la Mbeya.
Hapa upo juu kabisa Airpoint. Unalitazama Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Ukiwa hapo unaliona Bonde la Usangu kwa raha zako. Utayaona maeneo kama Inyala, Chimala, Igurusi, Itamba, Msesule na kadhalika. Utafurahia sana kuiona reli ya Uhuru inavyolizunguka eneo hilo.
Moja ya mambo niliyoyafurahia pahala hapo ni hali ya hewa yenye kusisimua mno.