Ni muda mrefu sana umepita tangu nilipoweka bandiko kwa mara ya mwisho hapa kibarazani kwangu. Marafiki zangu wamekuwa wakiniuliza mara kwa mara juu ya kupotea kwangu katika kublog.
Sikuwa na sababu ya msingi kuacha kuweka mabandiko. Ni kapepo tu ka-uvivu kalikoniandama.
Nimekakemea kwa nguvu zote.
Ninasikia furaha kusema, nimerejea kublog. Panapo majaaliwa, kwa picha na makala kadha wa kadha, kwa mtazamo wangu, Mwananchi Mimi.
Tuzidi kuwa pamoja.
Fadhy,
Mbeya, Tanzania.
Jumatano, Disemba 2, 2015.