Soma hii......
Mwanamke kashituka kutoka usingizini usiku wa manane na kugungua mumewe hayupo kitandani.
Mwanamke akachanganyikiwa na kuamua kushuka hadi chini. Akamkuta mumewe ameketi juu ya jikoni, kikombe cha kahawa kikiwa mbele yake huku akionekana kusononeka sana. Mwanamke akamtazama mumewe aliyekuwa akijaribu kujifuta machozi.
"Mume wangu una tatizo gani?" Akamwuliza huku akimsogelea. "Kwa nini upo huku usiku wote huu?"
Mumewe akauinua uso wake. Akamtazama. Kisha akamwuliza, "Unakumbuka miaka 20 iliyopita tulipokuwa tumeanza kuwa wapenzi tukiwa na umri wa miaka 17 tu?"
"Nkumbuka sana mume wangu. Jamani you are so sweet umenikumbusha mbali." Mwanamke akajibu huku akiubusu mkono wa mumewe.
"Unakumbuka jinsi baba yako alivyotufuma kwenye siti ya nyuma ndani ya gari langu?" Mwanaume akauliza kwa sauti ya tuo.
"Nakumbuka sana mume wangu!" Mwanamke akajibu huku akiketi sambamba na mumewe.
Mwanaume akaendelea kuongea. "Unakumbuka baba yako alivyonioneshea bastola yake kichwani mwangu na kuniambia aidha nikuoe, ama anipeleke jela miaka 20?"
Kwa sauti ya upole mwanamke akajibu, "Nakumbuka sana mume wangu. Tumepitia mengi mpenzi."
Mwanaume akanywa funda moja la kahawa. Kisha akaongea. "Leo ningekuwa natoka zangu jela.....na kuwa huru mtaani!"
Chanzo: Funny Jokes Tafsiri ya Kiswahili ni yangu.